Search This Blog
Monday, May 27, 2019
Ira yahukumu kunyongwa wanachama 3 wa dola ya Kiislamu
Mahakama moja jana Mei 26, iliwahukumu adhabu ya kifo raia watatu wa Ufaransa waliokuwa Wanachama wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu(Islamic State - IS).
Watuhumiwa hao, Kevin Gonot, Leonard Lopez na Salim Machou wamepewa siku 30 za kukata rufaa huku Mahakama ikisema kuwa imeshawahukumu zaidi ya wageni 500 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa IS tangu mwaka 2018.
Raia hao watatu waliohukumiwa jana ni miongoni mwa Wafaransa 13 waliokamatwa katika mapambano huko Mashariki mwa Syria na kukabidhiwa kwa mamlaka za Iraq mwezi Februari, 2019.
Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International, Iraq ndio nchi inayoongoza katika utekelezaji wa adhabu ya kifo duniani na ilitangaza kuanza kuliangamiza kundi la IS mwishoni mwa mwaka 2017.
http://bit.ly/2JHhFMm
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment