Search This Blog
Saturday, May 25, 2019
Dereva aliyemgonga Twiga Mikumi kupigwa faini Milioni 34
Dereva ambaye jina lake halijajulikana anayedaiwa kumgonga na kumuua mnyama Twiga katika mbuga ya wanyama ya Mikumi, Mkoani Morogoro amekimbia baada ya kufanya tukio hilo.
Anasteria Ndaga, Afisa Uhifadhi Wanyama Pori Kanda Ya Mashariki amesema mnyama huyo aligongwa jana saa tano asubuhi, ambapo wanalishikilia gari hilo pamoja na msaidizi wa dereva wa gari hilo na amefikishwa katika kituo cha polisi.
‘’Dereva wa gari hilo amekimbia na hajapatikana hadi leo, tunawasiliana na mmiliki wa gari ili taratibu zingine zitafuata za kisheria’’ amesema.
Ameendelea kwa kusema, "Sheria za Uhifadhi za Taifa, zinasema mnyama kama Twiga anapogongwa faini ni U$ Dollar elfu 15, sawa na Mill. 34 za Kitanzania, pia zipo gharama zingine za uharibifu wa mazingira, hatujampima kama alikuwa mjamzito’’.
http://bit.ly/2QmtUyp
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment