Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limesema linawapeleka watalaamu ili kuzuia unyanyasaji wa kingono katika nchi 10 zenye hatari kubwa ya uovu huo.Hatua hiyo inajiri baada ya kashfa kubwa kuripotiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako wahudumu wake na wafanyakazi wengine wa misaada waliwanyanyasa wanawake.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ametangaza mipango yake ya kuushughulikia mzozo huo wakati wa kikao cha faragha na wawakilishi wa mataifa 194 wanachama. Taarifa hiyo imesema mtalaamu mmoja tayari amekwenda Congo, lakini haikutaja mataifa mengine sita yanayoshuhudia kiwango kikubwa cha unyanyasaji wa wanawake.
Mwezi uliopita tume huru ilisema karibu wafanyakazi 83 wa misaada, robo yao wakiwa wa WHO, walihusika na unyanyasaji wa kingono wakati wa janga kubwa la Ebola kuanzia mwaka wa 2018 hadi 2020.
No comments:
Post a Comment