Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson hii leo ametembelea kanisa ambako mbunge David Amess aliuawa kwa kushambuliwa na kisu jana Ijumaa, katika tukio ambalo jeshi la polisi inalitaja kuwa la ugaidi.
Johnson, waziri wa mambo ya ndani Priti Patel na kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour Keir Starmer ni miongoni mwa viongozi walioweka shada za maua kwenye eneo hilo kama ishara ya kuomboleza kifo cha Amess. Taarifa ya polisi ya mapema leo imesema uchunguzi wa awali umeonyesha shambulizi hilo limechochewa na itikadi kali za Kiislamu.
Mtu mmoja aliyekuwa eneo la tukio anashikiliwa na polisi, wakimuhuisha na shambulizi hilo wanaloamini alilifanya peke yake.Amess ni mbunge wa pili kuuawa katika kipindi cha miaka mitano, wakati wakiwa nje kikazi kwenye majimbo yao, baada ya Joe Cox aliyeuawa kwa kupigwa risasi mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment