Takriban watu sita wameuawa na wengine 32 kujeruhiwa na risasi katika mji mkuu wa Beirut nchini Lebanon.
Yote haya yalianza wakati wa maandamano yaliofanywa na makundi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia , Hezbollah na Amal dhidi ya jaji mmoja aliyekuwa akichunguza mlipuko mkubwa mwaka jana katika mji huo wa bandari.
Walisema kwamba wanajeshi wa kuvizia wa dini ya Kikristo kutoka kwa jeshi la Lebanon LF walifyatua risasi katika kundi moja la watu kwa lengo la kuishinikiza Lebanon kuingia katika ghasia - madai yanayopingwa na jeshi hilo.
Hali ya wasiwasi inazunguka uchunguzi uliosababisha mlipuko huo uliowaua watu 219. Wapiganaji wa Hezbollah na washiriki wake wanadai kwamba jaji huyo anapendelea, lakini familia za waathiriwa wanaunga mkono kazi yake.
Hakuna hata mtu mmoja ambaye amepatikana na hatia kwa mlipuko huo wa Agosti 2020, ambapo maeneo mengi ya mji huo yaliharibiwa vibaya.
Akijibu mashambulizi ya siku ya Alhamisi , ambayo yamenonekana kuwa mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni, waziri mkuu Najib Mikati alitangaza siku ya kuomboleza siku ya Ijumaa.
Wakati huohuop, Rais Michel Aoun alisema: Hatutaruhusu mtu yeyote kuliteka nyara taifa hili kwa maslahi yao ya kibinafsi.
No comments:
Post a Comment