Search This Blog
Thursday, October 14, 2021
Wananchi wanena hatuna fedha za kuchangia maendeleo ila mchango wetu ni nguvu zetu acha tuchimbe msingi
Na Maridhia Ngemela,Mwanza
Wakaazi wa kata ya kayenze wamejitokeza kwa wingi kuchimba msingi wa kituo cha afya kinachotarajia kujengwa kwenye mtaa wa Nyabugali uliopo wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.
Hii ni baada ya serikali kupeleka sh milioni 250 kwa ajili ya kujenga kituo hicho ambacho kitapunguza changamoto ya wananchi kufuata huduma za matibabu mbali.
Wananchi hao wamejitokeza kuunga jitihada za Serikali kwa kuhakikisha wanachimba msingi huo bila kusubili wakandarasi wowote kutokana na uhitaji wa kituo hicho ambacho kitapunguza changamoto ya kufuata matibabu mbali hususani kwa mama mjamzito.
Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt.Angelinemabula alipokuwa katika zoezi la uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho kinachotarajia kuanza kijengwa hivi karibuni amesema ni vema kila mwananchi kuwa mwaminifu ili kuweza kupata kituo chenye ubora ambacho kitatoa huduma zote za matibabu.
" Tuendelee kumuunga mkono Rais kwa kusogeza karibu huduma za matibabu kwa wananchi ili kupunguza kero kwa jamii.
"Sisi kama wasaidizi wake na niwawakilishi wa wananchi tupo tayari kumuunga mkono ili kuhakikisha kila jambo ambalo amedhamilia kulifanya tutalisimamia katika utekelezaji wa shughuli hizo na kutambua matumizi ya pesa ili kupata kituo chenye ubora kinachokwenda na sera ya taifa.
Asemema mwaka 2019/2020 vituo viwili vya afya karume na Buzuruga viliboleshwa kwa sababu havikuwa na miundombinu kamili.
Amesema kituo hicho kikikamilika wilaya hiyo itakuwa na vituo vinne huku kata 15 zitakuwa hazina vituo hivyo lakini kwa jiografia ya mjini kituo kimoja kinaweza kuhudumia kata mbili hadi tatu.
"Bado tunauhitaji wa kuwa na Tarafa zaidi ya moja ili kusogeza huduma kwa wananchi kwani tuna kata 19 kuwa na tarafa moja bado ni changamoto lakini tunamshukru Rais kwa maamuzi yake ya matumizi mazuri ya tozo ambazo zimeendelea kutozwa katika mazingumzo yake alisema kila tarafa itapata kituo cha afya na sisi ni moja ya wanufaika wa fedhahizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Ilemela Modest Aplinary amesema kituo hicho kitakuwa na jengo la wagonjwa wa nje,maabara na kichomea taka ni vema wananchi kujitoa kwa hali na mali ili kuendelea kuokoa fedha ambazo zingetumika kulipa watu kuchimba msingi huo hata hivyo ametoa matofali 10,000 kwenye ujenzi huo
Mkuu wa Wilaya Hassan Masala amewapongeza wananchi kwa kuupokea mradi huo kwani atahakikisha fedha hizo hazikai kwenye akaunti na badala yake zinatafanya kazi ambayo imekusudiwa
ili kutatua changamoto kwa wananchi.
" Mtendaji msaidiane na kamati zilizoundwa tunataka kuona fedha hizi kuwanzia shilingi ya kwanza mpaka ya mwisho lazima zionekane kwenye karatasi imefanya jambo gani na kila iliyookolewa na wananchi kwa kujitolea itambulike imeokolewa kiasi gan lengo kupata zaidi ya haya majengo tatu kwa ukamifu ili kumuonyesha Rais tulikuwa na shida.
"Serikali ipo pamoja na nyinyi na itaendelea kuwa karibu na ikiwezekana kabla ya miezi tunatamani kituo hiki kiwe kimeanza kutoa huduma kwani fedha tunazo nguvu tunazo na nia tunayo na tumezionyesha hapa tunawashukru wananchi wote kwa kuupokea mradi huu na kutoa eneo sisi tutahalikisha fedha hazikai kwenye akaunti bali zinafanya kazi husika",alisema Masala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment