Search This Blog

Monday, October 18, 2021

Waandamanaji wanadai mapinduzi ya kijeshi Sudan mgogoro ukizidi kuongezeka


Wapinzani wa serikali ya mpito ya Sudan waliandamana katika barabaraza mji mkuu wa Khartoum Jumamosi kushinikiza jeshi kudhibiti nchi hiyo.

Maelfu ya watu kadhaa walikusanyika nje ya ikulu ya rais huku mgogoro wa kisiasa ukiendelea kuongezeka.

Jeshi na makundi ya kiraia yamekuwa yakigawana madaraka tangu Rais Omar al-Bashir alipong'olewa madarakani mwaka 2019.

Tangu wakati huo, viongozi wa jeshi wamekuwa wakidai mageuzi ya Umoja wa Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko (FFC), muungano wa raia ambao uliongoza maandamano ya kumpinga Bashir na kuunda sehemu muhimu ya serikali ya mpito. Vikosi vya wanajeshi pia vimetaka kubadilishwa kwa baraza la mawaziri.

Hata hivyoi, viongozi wa raia wanasema kuwa madai hayo ni njama ya kutaka kunyakua mamlaka kutoka kwa wanajeshi.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...