Search This Blog
Sunday, October 10, 2021
Ulega: "Mchezo wa bao uendelezwe kumuenzi Baba wa Taifa"
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, ambaye pia ni Waziri wa mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega ametoa rai kwa jamii kuuendeleza mchezo wa bao ili kumuenzi Muasisi wake, Baba wa Taifa ,Hayati, Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia 14,oktoba 1999.
Akimkaribisha mgeni rasmi katika fainali ya mchezo wa bao aliyoiandaa ili kumuenzi baba wa Taifa iliyofanyika Wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani ,Ulega alieleza ni muhimu kuendeleza michezo ya jadi ikiwemo mchezo wa bao kwani ni miongoni mwa michezo ambayo ni kielelezo cha Taifa.
Alisema jambo la kudumisha michezo ya jadi limesisitizwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umuhimu wa kurithisha utamaduni kwa watoto na kama tamaduni zetu hazitaenziwa zitapotea .
"Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anahimiza michezo, na kuenzi historia ya jadi sana, Zanzibar hawajawahi kuacha jadi yao hata mwaka mmoja ,ambapo kila mwaka kuna maonyesho ya jadi na mwaka huu yeye mwenyewe alikuwa kinara , kwenye michezo hiyo ya jadi maarufu kama Mwaka kogwa ili kudumisha masuala ya jadi,"alisisitiza Ulega
Pamoja na hilo ,aliwaasa wananchi kuendelea kudumisha amani na upendo ili kuendelea kumuenzi baba wa Taifa.
Ulega aliahidi kuendeleza mashindano ya mchezo huo kila mwaka ambapo safari hii alitenga milioni moja kwa washindi watatu ambapo mshindi wa Kwanza Vikindu walipatiwa kikombe na sh.500,000, Mwarusembe washindi wa pili 300,000 na Magawa 200,000 ambao ni washindi wa tatu.
"Washindi hawa watatu pia nimewaongeza 50,000 kila timu ili kununua bao mpya,"alifafanua Ulega.
Mcheza bao wa miaka mingi, Selemani Ndugugani alisema michezo hiyo ilianza mwaka 1975 na mwaka 1976 alianza kushiriki michezo hiyo hadi mwaka 1980.
"Michezo hii ya jadi inaonekana kufa lakini tunamshukuru mbunge Ulega kufufua huu mchezo wa bao, unafaida kama soka tu, miaka hiyo mimi mchezo huu ulinifikisha mikoani ya Musoma, Bukoba na Lindi ," alisema Ndugugani
Alimuomba Ulega kuzungumza na wizara ya Utamaduni kuenzi michezo hii na sio soka pekee.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Hadija Nasir alisema mchezo wa bao unaimarisha akili na kuleta furaha .
"Mwanzilishi wa mchezo huu hayat Mwl.Nyerere alidumisha mchezo huu na sisi tunapaswa kuuenzi, " alisema Nasir
Mashindano hayo yalianza ngazi za vijiji na kuunda mashindano ya kata hadi Tarafa na kufuzu kuingia robo fainali .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment