Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza mipango ya kuzindua mtandao mpya wa media ya kijamii, uitwao TRUTH Social.
Amesema jukwaa hilo "litakabiliana na jeuri ya kampuni kubwa za teknolojia ", akizishutumu kwa kunyamazisha sauti za wapinzani huko Marekani.
Kampuni ya Trump Media & Technology Group (TMTG), ambayo yeye ni mwenyekiti wake, pia inakusudia kuzindua huduma ya usajili wa mahitaji ya video.
Bw. Trump alipigwa maarufuku katika mitandao ya kijamii au kufungiwa na mitandao kama ya Twitter na Facebook baada ya kundi la wafuasi wake kuvamia Bunge la Marekani Januari mwaka huu.
Yeye na washauri wake tangu wakati huo walidokeza kuwa wanapanga kuunda mtandao hasimu wa kijamii.
Mapema mwaka huu, alizindua Kutoka kwa Dawati la Donald J Trump, ambayo mara nyingi ilikuwa ikiitwa blogu.
No comments:
Post a Comment