Search This Blog

Monday, October 4, 2021

Tetesi za soka kimataifa


Atletico Madrid imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji Timo Werner, 25 anayekipiga Chelsea. (Transfer Market Web)

Mkurugenzi wa Fiorentina Joe Barone amesema klabu inafanya ''jitihada kubwa'' kuongeza mkataba wa Mserbia Dusan Vlahovic, huku mkataba wa sasa ukitarajiwa kumaliza mwezi Juni mwaka 2023.(DAZN, via Football Italia)

Mlinzi wa Ivory coast Serge Aurier, 28, ambaye sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Tottenham Hotspurs, anajiandaa kujiunga na Villarreal ya Uhispania.(L'Equipe - in French)

Manchester City wanamfuatilia kiungo wa kati wa Uhispania Nico Gonzalez anayekipiga Barcelona, ambaye hajapewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza . (Fichajes - in Spanish)

Wakati huohuo, mlinzi Sergi Roberto ni mchezaji mwingine wa Barcelona anayetolewa macho na Manchester City, wakati mkataba wa mchezaji huyo huko Nou Camp ukitarajiwa kumalizika majira ya joto yajayo. Calciomercato - in Italian)

Claudio Ranieri amekubali kuwa kocha mkuu mpya wa Watford baada ya kuondoka kwa Xisco Munoz siku ya Jumapili, huku Muitaliano huyo, 69 akitarajiwa kuweka saini Jumatatu. (Sky Sports)

Mlinzi kinda wa Kijerumani anayecheza katika klabu ya Borussia Monchengladbach Luca Netz anadai alikataa uhamisho aliosema ''hauna maana'' kwenda Manchester City miaka mitatu iliyopita, mchezaji huyo mwenye miaka 18 anasema atawakatalia kwa mara nyingine tena. (Sun)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Alexis Sanchez hajui mustakabali wake Inter Milan baada ya mchezaji huyo mwenye miaka 32-kuchapisha kisha kufuta ujumbe uliokuwa ukikosoa kitendo cha kukosa muda wa kucheza uwanjani. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure, 38, ametoa ofa kwa Barcelona wakati huu wakiwa katika changamoto, lakini haijulikani kama raia huyo wa Ivory coast anataka kucheza au kufundisha. (Sun

Atletico Madrid nayo imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji Timo Werner, 25 anayekipiga Chelsea. (Transfer Market Web)

Mmiliki Mike Ashley anajua njia pekee ya kumbadili kocha mkuu wa Newcastle ni kulipa karibu kila kandarasi ya Steve Bruce ambayo alikubali mnamo Julai 2019.(Chronicle Live)

Mshambuliaji wa Kiholanzi anayecheza Bayern Munich Joshua Zirkzee, 20, anasema alikataa nafasi ya kujiunga na Everton mwaka 2017. (Het Nieuwsblad via Liverpool Echo)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...