Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha kuna wigo mpana wa miundombinu ya upatikanaji huduma za afya ya uzazi CEmONC karibu zaidi na wananchi mathalani vituo vya afya 487 vinatoa huduma hizi .
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa 26 wa mwaka wa AGOTA uliofanyika Mkoani Dar es Salaam.
Wizara yangu inatambua mchango mkubwa AGOTA hapa nchini katika kuboresha huduma za uzazi hususan katika kuhakikisha wajawazito wote wanapata huduma bora katika kipindi chote cha ujauzito, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua na wale wanaohitaji huduma za dharura za uzazi wanaweza kujifungua salama ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Wizara inazo taarifa zenye ushahidi wa kutosha kuhusu utendaji wenu wa kujenga uwezo wa watumishi wa kada za chini kwa kutumia mfumo wa mafunzo kazini kwenye stadi na ujuzi wa kupambana na dharura za uzazi za kuokoa maisha ya mama na mtoto alie tumboni.
Tumeona mkisaidiana na wizara kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Singida, Tabora, Dodoma, na mingine katika kujenga uwezo wa watumishi kupambana na dharura kwa njia anuai ikiwamo za upasuaji ulio salama. Napenda kuwahakikishia hapa leo kuwa Wizara inathamini sana mchango huu.
No comments:
Post a Comment