Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameanza maandalizi ya kuwachanja chanjo ya polio watoto wa umri wa chini ya miaka mitano katika maeneo yote ya Afghanistan baada ya mamlaka ya Taliban kukubali kuanza upya utekelezaji wa chanjo hiyo.
Hii ni hatua mpya ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza tangu 2018. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Taliban iliyazuia mashriki hayo katika maeneo wanayoyadhibiti kwa hofu ya kwamba huenda ikiwa mbinu ya upelelezi inayofanywa na iliyokuwa serikali ya Afghanistan au mataifa ya Magharibi.
Kutokana na marufuku hiyo na mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea nchini humo, takribani watoto milioni 3.3 wamekosa fursa ya chanjo.
Hatua hiyo ya utawala wa Taliban, ambayo inachukuliwa katika kipindi ambacho kiwango cha polio kikizidi kuongezeka nchini humo kinaoensha ishara ya serikali hiyo mpya kuwa tayari kushirikiana na jumuiya ya kimatiafa.
No comments:
Post a Comment