Search This Blog

Thursday, October 14, 2021

Skauti Songwe kumuenzi Nyerere kwa kutoa Elimu ya Uzalendo kwa watoto wadogo



Na  Baraka Messa

 

SKAUTI Mkoa wa Songwe wamejipanga kumkumbuka na Kumuenzi Baba wa Taifa Hayati mwalimu Julias Kambalage Nyerere kwa kutoa elimu na kuhamasisha watoto wadogo kuanzia miaka mitano kujiunga na Skauti ili kujifunza maadili uzalendo na ujenzi wa kazi za Taifa .

 

hayo yamebainishwa na Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Songwe Edmund Mwakambonja  alisema skauti iliasisiwa na Mwalimu Nyerere baada ya Uhuru kwa lengo la kuimalisha ulinzi, uzalendo, kuibua matendo maovu ya rushwa na vijana kujifunza kazi nzuri za ujenzi wa Taifa.

 

Alisema wamejipanga kuwafikia watoto wadogo kuanzia  miaka mitano ambao wanasoma awali na shule za Msingi ili wajiunge na skauti ambapo kulingana na umri wao watajifunza nyimbo za uzalendo zinazohamasisha amani na kukemea maovu mbalimbali.

 

"Rais wa Skauti Taifa ni Waziri wa Elimu ambaye atakuwa madarakani kwa kipindi hicho, ngazi ya Mkoa kiongozi wa Skauti ni Afisa Elimu Mkoa na ngazi ya wilaya ni Mkuu wa wilaya  husika , hivyo tunaomba wapewe ushirikiano na kupata malezi mazuri ili waendelee kutusaidia Skauti ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wazazi kuruhusu watoto kujiunga " alisema Mwakambonja.

 

Kwa upande wake Kamishna wa  Skauti Mkoa wa Songwe Osward Mshani alisema alisema watoto wa miaka mitano mpaka miaka kumi wanapewa mafunzo yao kulingana na umri wao, ambapo ikiwa ni pamoja na nyimbo, kuchora na kujifunza na kupewa nishani pindi wanapofanya vizuri.

 

Afisa elimu Mkoa wa Songwe Juma Kaponda alisema mtoto mdogo ubongo wake ni mwepesi kujifunza hivyo aliwataka wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Songwe kutekeleza na kuwasimamia vizuri vijana wa skauti kutokana na umuhimu wao katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na utunzaji Mazingira pamoja na kupambana na vitendo viovu.

 

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...