Search This Blog

Saturday, October 16, 2021

Samia: Nitawahudumia Watanzania kwa jicho la huruma


Rais Samia Suluhu Hassan amesema ataendelea kuwahudumia Watanzania kwa jicho la huruma na kadiri Mungu atakavyomuwezesha.

Rais ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Oktoba 16, 2021 wakati wa ibada ya shukrani ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Jubilei ya Hospitali Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).

“Niungane na Askofu Shoo alivyosema kwamba kila mmoja wetu atumie kalama tulizojaaliwa na mwenyezi Mungu katika kutoa huduma kwa wananchi,  nami kwa upande wangu kama ulivyoniomba Baba Askofu nitaendelea kuhudumia Watanzania jinsi na kadiri Mungu atakavyoniwezesha,  nitaendelea kuwatazama Watanzania kwa jicho la huruma kama lilivyojicho langu na jinsi Mungu atakavyoniwezesha naomba mniombee na mnipe msaada na  ushirikiano mkubwa ili kazi ya kuendesha Taifa hili liwe rahisi kwangu,” Rais Samia Suluhu Hassan.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...