Ndege hizo mpya moja itapewa jina la Zanzibar na nyingine Tanzanite.
“Ndege hizi zina mfumo wa kisasa na zimeongezewa uzito hasa wakati wa kuruka kutoka Tani 67 hadi kufikia tani 69.9 lakini pia ina viti vya kisasa ambavyo vitawafanya abiria kustarehe zaidi” amesema Profesa Mbarawa.
Ujio wa ndege hizo utaifanya Tanzania sasa kuwa na ndege 11.
Amefafanua kuwa, pia ndege hizo zitakuwa na burudani za watoto, muziki, sinema na internet na hivyo kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwa maendeleo ya nchi .
No comments:
Post a Comment