Search This Blog

Saturday, October 9, 2021

Rais wa kwanza wa Iran Abolhassan Banisadr afariki


 Rais wa kwanza wa Jamhuri ya watu wa Iran Abolhassan Banisadr amefariki dunia leo Jumamosi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali moja mjini Paris, Ufaransa. Amefariki akiwa na umri wa miaka 88. Kifo cha rais huyo wa zamani wa Iran kimethibitishwa na shirika la habari la Iran IRNA. 


Kwa mujibu wa familia yake, ameaga dunia baada ya maradhi ya muda mrefu. Abolhassan Banisadr, alikuwa rais wa kwanza wa Iran baada mapinduzi ya kiislamu 1979 na aliikimbia nchi yake na kuishi uhamishoni Ufaransa baada ya kushtakiwa kwa kuwapinga viongozi wa kidini walioonekana kuwa na nguvu zaidi wakati huo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...