Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera ametangaza kusitishwa vita kutokana na machafuko ya muda mrefu kati ya serikali na waasi, huku akisema makundi mawili makubwa yenye silaha yamekubali kuacha vita.
Kwenye tangazo lake kupitia kituo cha radio kinachomilikiwa na serikali, Touadera amesema hatua hiyo ya usitishaji vita mara moja inaashiria dhamira yake ya kuyapa mazungumzo ya amani kipaumbele baada ya miaka minane ya machafuko.
Taifa hilo lilitumbukia kwenye vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe baada ya mapinduzi ya mwaka 2013.Japo machafuko yamepungua katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, makundi yenye silaha bado yanadhibiti sehemu kubwa za nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment