
Papa Francis amezindua kile ambacho wengine wanakielezea kuwa ni jaribio kubwa zaidi kuweza kufanyika katika mabadiliko ya kanisa katoliki kwa miaka 60.
Miaka miwili ya mchakato wa kupata ushauri kutoka makanisa yote ya kanisa katoliki duniani kuhusu mwelekeo wa kanisa hilo kwa siku zijazo umeanza Vatican mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya waumini wa Katoliki wanamatumaini kuwa mabadiliko yanweza kugusia mambo kama wanawake kuongoza ibada, mapadre kuoa na mahusiano ya jinsia moja.
Wengine wakihofia mabadiliko hayo yataathiri misimamo ya kanisa katoliki.
Wanasema suala la kuzingatia kufanya mageuzi kunaweza kuathiri masuala mengine yanayolikabili kanisa kama rushwa na kupungua kwa idadi ya waumini.
Papa Francis amewataka wakatoliki kusikilizana na kuacha kuweka vizuizi.
No comments:
Post a Comment