Search This Blog

Monday, October 11, 2021

Naombeni mnisaidie nimeteseka zaidi ya miaka 10- Felista


Na Maridhia Ngemela,Mwanza  

Nimelala hapa kitandani zaidi ya miaka 10 nakutegemea familia yangu inihudumie kila kitu naiomba Serikali inisaidie nateseka na huu ugonjwa.

Rais  wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameombwa kutoa msaada wa hali na mali ili kuweza kunusulu maisha ya  Felista  Edward ambaye ni mgonjwa  kwa zaidi ya miaka 10  akiwaamelala  kitandani bila kuamuka kwa sababu ya kusumbuliwa na bandama na kupelekea tumbo kuvimba na miguu.

Mgonjwa huyo ambaye ni  mkazi wa  mtaa wa  mchongomani uliyopo  wilayani Ilemela  Mkoani Mwanza alisema amelala kitandani  zaidi ya 10 kwa sababu ya  kuugua ugonjwa huo.

"Tangu nilipoanza kuugua ugonjwa huu ninamiaka 21  ila nilikuwa sijazidiwa  hivi lakini ninamiaka zaidi ya 10 nipo kitandani  siwezi kifanya kitu chochote na nimetibiwa  hospitali ya  rufaa ya mkoa ya Sekou toure  lakini  sasa hivi sina fedha ya matibabu zaidi ya kununua vidonge kwenye maduka tu.

"Nimevimba  kuvimba tumbo na miguu na siwezi hata kukaa wala kujigeuza naomba wananchi na viongozi mbalimbali waweze kunisaidia fedha za matibabu ili niweze kwenda  kutibiwa  kwenye  hospitali kubwa kama mnavyoniona hapa nateseka hakuna kitu kinaumiza kama kumtegemea kufanyiwa kila kitu.",alisema Felista.

Naye  Kassimu  Masota ambaye ni mume  wa mgonjwa  huyo alisema kwa hivi sasa hawezi kufanya kazi yoyote  zaidi ya kumuuguza  mke wake  jambo ambalo linapelekea familia kukosa kipato cha kujikimu kimaisha.

 "Naomba msaada wa hali na mali  kwa jamii na serikali ili niweze kumtibu  mke wangu   ambaye amelala kitandani  zaidi ya miaka 10 bila kupata nafuu kwa hivi sasa hawezi kukaa wala kutembea na tumbo na miguu vimevimba.

"Kupitia kuuguliwa na mke wangu nina mtihani  mkubwa kwani  uwezo wa kununua chakula, maji sina na vyote vinahitajika na hivi sasa sifanyi kazi yoyote zaidi ya kuuguza  nawaombeni msaada wenu,"alisema Masota.

Mwalimu Tatu Ngelangela  ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kilimahewa alisema   baada ya kutomuona mwanafunzi wake   shuleni hapo kwa mda mrefu ndipo alipofatilia na kubaini tatizo hilo.

"Nilipoona  mwanafunzi wangu haji shuleni nilimfatilia na kubaini  anaishi na bibi yake ambaye anatatizo hili  nilichukua jukumu la kuwaita waandishi ili waweze kumsaidia apate msaada  wa matibabu.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...