Search This Blog

Monday, October 11, 2021

Mwalimu wa Quran aamuru wanafunzi kuchapa wanafunzi wenzao


Serikali ya Nigeria katika jimbo la Kwara imesema imemsimamisha mkuu wa shule ya Quran katika jimbo hilo baada ya video kusambaa ikionesha makundi ya wanafunzi wakiwa wanaadhibiwa kwa kutokuwa na nidhamu.

Baadhi ya wanafunzi hao ambao walikuwa wanaume na wanawake walishutumiwa kunywa pobe katika sherehe ya kuzaliwa ya mwanafunzi mwenzao.

Wanafunzi hao wanadai walikunywa maziwa ya mtindi tu.

Hata hivyo waliendelea kupigwa na wanafunzi wenzao ambao walikuwa wanapewa amri na mwalimu wa Quran.

Video moja ambayo ilisambaa mitaoni na kuonekana na BBC, inawaonesha wanafunzi wa kike wakiwa wamepiga magoti wakati wakipigwa fimbo na wanafunzi wa kiume na wengine wakiwa wanatazama.

Kamishna wa elimu na maendeleo alitoa taarifa Jumapili ma kusema wanafunzi hao wamepelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya na matibabu.

Taarifa ya serikali inayotaka uchunguzi ufanyike dhidi ya tukio hilo na adhabu kali zinazotolewa shuleni.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...