Search This Blog

Thursday, October 7, 2021

Mpinzani maarufu wa ubaguzi wa rangi Desmond Tutu atimiza umri wa miaka 90

Matukio mbali mbali yanafanyika nchini Afrika Kusini kuadhimisha mwaka wa 90 wa kuzaliwa kwa mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel, Desmond Tutu.

Anatarajiwa kuhudhiria misa katika kanisa kuu la St George katika mji wa Cape Town, ambako alihuudumu kama Askofu mkuu wa kwanza mweusi nchini humo katika miaka ya 1980.

Dalai Lama na Graca Machel, mjane wa hayati rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, ni miongoni wale ambao wanatarajiwa kushiriki katika mhadhara wa mtandaoni kwa ajili ya heshima ya Askofu Tutu.

Ingawa kwa kiasi kikubwa aliondoka katika maisha ya umma muongo uliopita, Desmond Tutu atakumbukwa kwa uongozi wake katika kupinga utawala wa wazungu wachache katika enzi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Hivi karibuni, aliunguza dhidi ya ufisadi na gasia za ubaguzi dhidi ya wageni.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...