Search This Blog

Sunday, October 10, 2021

Merkel akutana na Naftali Bennet Israel


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett kwa mazungumzo hii leo, ikiwa ni ziara yake ya mwisho rasmi nchini Israel. 


Baada ya kukutana na Bennett, kansela huyo anapanga kukutana na Rais wa Israel Isaac Herzog na Waziri wa Kigeni Yair Lapid kwa mara ya kwanza tangu kuundwa serikali mpya. 


Merkel pia atakutana na baraza la mawaziri la Israel. Mada anazotarajiwa kuzijadili Merkel katika ziara yake hiyo ni pamoja na mpango wa nyuklia na Iran, suala la Palestina iliyo huru, pomoja na uhusiano kati ya Ujerumani na Israel. 


Kufuatia uchaguzi wa Septemba, Merkel anatarajiwa kuachia ngazi mara tu baada ya serikali mpya kuundwa Ujerumani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...