Search This Blog

Saturday, October 23, 2021

Maua Sama anunua gari nyingine


Hakika huu ni mwaka wenye neema kwa Maua Sama kwasababu licha ya ngoma zake kufanya vizuri kupitia digital platforms mbalimbali pia amefanikiwa kulamba madili makubwa ya ubalozi ikiwemo UBALOZI wa TPB Bank.

Maua ambaye hivi karibuni alitangaza kuwa amepona matatizo yaliyokuwa yakimsumbua kwa takribani miezi saba ya kusikia pamoja na kinywa, mbali ya kuwa msanii pia amesomea mambo ya masoko 'marketing'.

Sasa good news ni kwamba tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka 2021, Maua Sama ameamua kuvuta ndinga (gari) yake mpya aina ya Toyota Vanguard. Maua ame-share habari hiyo njema na mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa instagram.

Kwasasa Maua anakuwa ameongeza listi ya magari yatakayo patikana kwenye parking yake. 


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...