Search This Blog

Tuesday, October 5, 2021

Mashirikiano baina ya serikali na sekta binafsi kumechangia kuongezaeka kwa watalii


NA THABIT MADAI,ZANZIBAR

IMEELEZWA kuwa, Mashirkiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Sekta binafsi husani wamiliki wa Hoteli kumechangia kwa kiasi kikubwa kukuza Sekta nzima ya utalii wa Zanzibar.

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wamiliki wa Hoteli Zanzibar (HAZ), Paulo Rosso aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa zoezi la upigaji wa chanjo ikiwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Uviko 19 ambao ni tishio.

 

Alisema kuwa, kuwepo kwa Mashirikiano hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kukuza sekta nzima ya utalii ikiwemo kuchangia ongezeko la watalii kutoka mataifa mbalimbali.

 

“Sisi kama Jumuiya ya Wamiliki wa Hotel (HAZ) tunapongeza sana Serikali kwa kuweka mashirikiano na sisi Sekta binafsi ambayo yamechangia ukuzaji wa Utalii”,alisema.

 

Alisema takwimu zinaonesha kuwa licha ya kuwepo kwa janga la Covid 19 bado sekta nzima ya utalii nchini bado inaimarika na wamekuwa wakipokea watalii kutoka nchi mbalimbali.

 

“Kutokea Mwaka 2019, 2020 wakati dunia imeshamiri kwa janga la Corona bado takwimu inaonekana kuwa utalii wa Zanzibar bado unaimarika kwa watalii mbalimbali kutembelea Zanzibar,” alisema.

 

Hata hivyo, aliahidi kuendelea kufanya kazi kwa nguvu zote ili kufanya Zanzibar kuwa kitovu cha Utalii pamoja na kuwa Nchi ambayo inatembelewa na watalii wengi Duniani.

 

Sambamba na hayo, alisema kuwa Sekta ya utalii nchini hupelekea kuzalisha kwa ajira nyingi kwa wananchi hususani vijana.

 

“Katika kuliona hilo sisi HAZ tunafanya kazi na Taasisi nyingine za Serikali na binafsi ili kuitangaza Zanzibar na vivutio vyake”,alisema.

 

Hata hivyo, alimpongeza Juhudi zinazofanywa na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kufungua milango kwa wawekezaji kuja kuwekeza Zanzibar ambapo, alisema hatua hiyo itasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa haraka.

 

Mapema wafanyakazi wa hoteli ya Sandies bao bao beach Zanzibar iliyoko nungwi wamepatiwa chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa covid 19

 

Akizungumza katika zoezi hilo, Human Resources wa hoteli hiyo, Beatrice Julius Musomi, alisema kupatiwa chanjo hiyo kutawasaidia kujikinga na ugonjwa wa Uviko 19 kwani wao ndio wanaowapokea wageni wanaokuja katika hoteli yao.

 

Aidha aliushukuru uongozi wa Hoteli hiyo kwa kuona ni vyema kuwapatia chanjo hiyo sambamba na kuwataka wannachi kuendelea kuiunga mkono juu ya suala la upigaji wa chanjo ili kuendelea kujikinga na ugonjwa.

 

“Wananchi wenzangu ni vyema tukaendelea kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga chanjo kwani itasaidia kujikinga na ugonjwa kwani ugonjwa huu ni tishio la taifa” alisema.

 

Mmiliki wa hoteli hiyo Paulo roso, alisema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kufungua fursa ya uingizaji wageni kutoka mataifa mbali mbali ili kukuza soko la utalii.

Alisema, kwa sasa baadhi ya nchi ikiwemo Itali hawaingii nchini kwa kuhofia afya zao ambapo ndio wanaoingia fedha nyingi kupitia utalii hivyo hatua hiyo itahamasisha watalii hao kuingia nchini na kukuza uchumi wa nchi.

 

“Tutaendelea kuiunga mkono serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi wake Dk. Hussein Mwinyi kwa kuwa nasi karibu wawekezaji ili kuendelea kuutangaza utalii wa Nchi sambamba na kuleta wageni nchini” alisema.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...