Kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS limedai kufanya shambulizi kwenye msikiti wa Kishia katika mji wa Kandahar, kusini mwa Afghanistan jana. Kwenye shambulizi hilo karibu watu 47 waliuawa.
Taarifa iliyochapishwa kwenye shirika lake la habari la Amaq imesema, washambuliaji wake wawili wa kujitoa muhanga waliwaua walinzi wa msikiti kabla ya kulipua mabomu waliyokuwa wameyavaa katikati ya kundi la zaidi ya watu 300 waliokuwa kwenye sala ya Ijumaa.
Afisa mmoja wa Taliban ameliambia shirika la habari la DPA kwamba watu 47 wamekufa kwenye shambulizi hilo na wengine karibu 70 walijeruhiwa.
Kundi la IS ni madhehebu ya Sunni wanawaona Washia kama waumini wanaokufuru, lakini pia ni wapinzani wakubwa wa kundi la Taliban linaoongoza serikali mjini Kabul, licha ya kuwa wote ni waislamu wa madhehebu ya Sunni.
No comments:
Post a Comment