Search This Blog

Thursday, October 7, 2021

Kiongozi wa mapinduzi Guinea amteua waziri mkuu mpya

Kiongozi wa jeshi la Guinea amemtaja mfanyikazi wa zamani wa serikali Mohamed Beavogui kama waziri mkuu kusimamia mabadiliko ya utawala wa raia kufuatia mapinduzi ya mwezi uliopita.

Bwana Beavogui, 68, ni mtaalam wa fedha katika sekta ya kilimo. Ana uhusiano wa kifamilia na mwanadiplomasia wa zamani wa Guinea ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa kwanza wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika, ripoti za mashirika ya habari zinasema.

Uteuzi wake ulitangazwa Jumatano katika amri iliyosomwa kwenye runinga ya taifa .

Kiongozi wa mapinduzi Kanali Mamady Doumbouya Ijumaa iliyopita aliapishwa kuwa rais wa mpito.

Amezuiwa kugombea uchaguzi wa baadaye chini ya mipango ya kurejesha utawala wa kiraia. Aliahidi kuandaa uchaguzi huru , wa kuaminika na wa uwazi lakini hakusema utafanyika lini.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...