Search This Blog

Tuesday, October 12, 2021

Kim Jong Un ailaumu Marekani kwa kusababisha wasiwasi kwenye rasi ya Korea

 


Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un ameitupia lawama Marekani kwa kuwa chanzo cha wasiwasi katika rasi ya Korea.Kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini hii leo, Kim Jong Un ametoa lawama hizo kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho ya kijeshi akisema Marekani ndio chanzo hasa cha kukosekana kwa ustahmilivu kwenye eneo hilo.

Kim Jong Un amesema serikali ya rais Joe Biden imekuwa ikisema haina ugomvi na Korea Kaskazini lakini ana wasiwasi mkubwa kama kuna watu ama taifa linaloamini hilo.

Kiongozi huyo amesema hakukuwa na msingi wowote wa Marekani kuchukua hatua dhidi yake iwapo hakuna mvutano kati yao. 

Aidha Kim ameilaumu Korea Kusini kwa undumila kuwili akisema majaribio yake hatari ya kujiimarisha kijeshi yanavuruga usawa wa kijeshi katika rasi ya Korea na kuongeza hali ya wasiwasi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...