Search This Blog

Sunday, October 10, 2021

Kansela wa Austria kujiuzulu kwa kashfa ya rushwa


Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu Alexander Schallenberg amesema amechaguliwa na Kansela wa Austria Sebastian Kurz kumpokea nafasi yake nafasi yake kama kansela wa nchi hiyo. Hayo yanajiri baada ya Kurz kutangaza kuwa atajiuzulu kutokana na shinikizo la kuhusishwa na tuhuma za ufisadi. 


Kurz mwenye umri wa miaka 35, aliyeingia madarakani 2017 amesema anafanya hivyo ili kuepusha vurugu. Kurz amechukua hatua hiyo baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa Austria kusema Kansela Kurz na watu wengine tisa walikuwa wakichunguzwa kwa rushwa baada ya wapelelezi kufanya msako katika ofisi za chama tawala. 


Wote hao kwa pamoja wanachunguzwa kwa tuhuma ya kutumia pesa ya serikali katika kipindi cha kati ya miaka ya 2016 na 2018 kuvihonga vyombo vya habari kuwaandika vizuri. Hata hivyo, Kurz amesema tuhuma zote dhidi yake ni za uongo, na kwamba yupo tayari kuzitolea ufafanuzi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...