Majaribio ya hivi karibuni ya makombora yanaonesha kwamba Korea Kaskazini ina mpango wa kutengeneza silaha wa mara kwa mara.
Korea Kaskazini inasema kuwa inahitaji kutengeneza silaha kwa ajili ya kujilinda na mashambulio yanayoweza kufanywa na Marekani dhidi yake.
Jumanne wiki hii Korea Kaskazini ilisema ilifanikiwa kufanya majaribio ya kombora lake aina ya hypersonic.
Kombora hilo, lililoitwa jina Hwasung-8, ni mojawapo ya mifumo yake ya '' silaha tano muhimu'' zilizotengenezwa chini ya mpango wa kijeshi wa miaka mitano, vilisema vyombo vya habari vya taifa hilo.
Hili ni jaribio la tatu la kombora kufanywa katika Korea Kaskazini ndani ya mwezi mmoja.
Awali, Korea Kaskazini ilifanya jaribio lake mapema la masafa marefu kwa kutumia teknolojia mpya inayowezesha kombora kuongozwa na kusafiri kwa masafa marefu kwa mwendo upiopangwa na kupiga maeneo yaliyolengwa.
Mwezi Januari, Korea kaskazini ilifichua kombora linaloweza kufyatuliwa kutoka majini ambalo ililitaja kama silaha yenye nguvu zaidi dunaini.
Uwezo wa silaha wa taifa hili haujulikani na hauko wazi iwapo kutokana na kwamba baadhi ya silaha bado hazijafanyiwa majaribio.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa ataongeza uwezo wa nchi yake wa kijeshi.
Huku ikikumbwa na vikwazo vya kiuchumi, Korea Kaskazini imeongeza kwa kiasi kikubwa cha uwezo wake wa kijeshi
Makombora yanayofika Marekani
Makombora yaliyojaribiwa na Korea Kaskazini katika kipindi chote cha mwaka 2007 yanaonesha kupiga hatua kubwa katika teknolojia yake ya kijeshi.
Kombora la Hwasang-12 lilikadiriwa kuwa na uwezo wa kupiga masafa ya kilomita 4,500 na linaweza kupiga ngozme za kijeshi za marekani ziliopo katika kisiwa cha Guam.
Kombora aina ya Huasang-14 baadaye lilionekana kuwa lenye nguvu zaidi, likiwa na uwezo wa kupiga eneo lililopo umbali wa kilomita 8,000 na kuweza kufika kilomita 10,000.
Lilikuwa ni kombora la kwanza la Korea Kaskazini la aina ya ballistic linaloweza kupiga nje ya Korea na lenye uwezo wa kupiga New York.
Kombora aina ya Hwasang-15 lilipaswa kupaa umbali wa kilomita 4,500 kwenda juu . Umbali huu ni mara 10 juu zaidi ya mahali kilipo Kituo cha kimataifa cha anga za mbali .
Kombora hili linapiga kwenye ardhi, linaweza kufika hadi kima cha kilomita 13,000, hii ikimaanisha kuwa lina uwezo wa kufika kokote nchini Marekani.
Mwezi Oktoba 2020, Korea Kaskazini ilifichua kombora la ballistic lisilojulikana. Kombora hilo ambalo halijafanyiwa majaribio linasemekana kuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya silaha moja ya nyuklia.
Mwezi Machi, Kora Kaskazini ilisema kuwa ilikuwa imetengeneza kombora lingine lenye uwezo wa Kubeka kilo 2,500 za silaha. Hii inamaanisha kuwa linaweza kubeba silaha za nyuklia.
Makombora yanayoweza kusafiri kwa kuongozwa na kuweza kulenga maeneo hata yaliyojificha, ambayo yamejaribiwa, yanasemekana kuleta changamoto kwa mifumo ya ulinzi dunaini.
Baraza la uslama la Umoja wa Mataifa limepiga marufuku Korea Kusini isijaibu makombora yake ya ballistic, lakini haijakoma kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu.
Kombora la hypersonic lililojaribiwa Jumanne lina kasi kubwa.
Bomu la Thermonuclear
Tarehe 3 Septemba, 2017, Korea kaskazini ilifanya jaribio lake kubwa zaidi la nyuklia ambalo halijawahi kufanyika hadi sasa.
Nguvu ya mlipuko wa kifaa hicho ina ukubwa wa kilo za tani 100 hadi 370.
Bomu la kila za tani 100 lina nguvu mara sita zaidi ya lili lililangushwa katika Hiroshima mwaka 1945.
Korea kaskazini imedai kuwa ilikuwa inajaribu silaha yake ya kwanza ya thermonuclear. Baada ya silaha ya nyuklia kulipuliwa na atomi, mlipuko mwingine umetengenezwa kusababisha mlipuko mkubwa zaidi.
Aprili 2018, Korea Kaskazini ilisema kuwa itaacha kufanya majaribio ya nyuklia pale uwezo wake utakapothibitishwa.
Ilisema itaharibu eneo lake la majaribio ya silaha zake za nyuklia na kuharibu baadhi ya miundo mbinu mbele ya baadhi ya waandishi wa habari wa kimataifa . Lakini wataalamu hawakuwepo wakati huo .
Baada ya kuwasiliana na aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump mwaka huo, Korea Kaskazini ilisema kuwa itafunga miundombinu yote ya mpango wa nyuklia. Lakini mazungumzo baina ya Trump na Kim Jong-un hayakuweza kuzaa matunda.
Mwezi Agosti, Shirika la Umoja wa Mataifa la udhibiti wa nishati ya lilisema kuwa Kotrea imefufua kazi za nyuklia.
Mwezi Septemba, Kprea Kaskazini ilisema kuwa mpango wake wa nyuklia unaendela kikamilifu
Korea Kaskazini ina idadi kubwa ya wanajeshi. Inakadiriwa kuwa kuna zaidi ya wanajeshi milioni moja walio kazini na wengine wengine zaidi ya milioni sita wa akiba.
Ingawa nyingi kati ya silaha zake zimepitwa na wakati na hazitumiki, Korea Kusini yenye jumla ya wanajeshi 600,000 ndio inayoweza kupata hasara kubwa iwapo kutatokea vita baina ya nchi hizo kutokana na idadi yake ndogo ya wanajeshi
Tisho jingine ni kwamba nchi hiyo ina zaidi ya azina za silaha 31,00, kama vile miitambo ya kufyatua maroketi, ambayo yanaweza kupiga, iliyopo umbali wa maili 60.
Katika mwaka 2012, Korea Kusini ilikadiria kuwa Korea Kaskazini ina tani kati ya 2,500 hadi 5,000 za silaha za kemikali, ikiwa huenda ndio hifadhi kubwa zaidi ya silaha hizo duniani.
Inasemekana kuwa mpango wa silaha za kibaiolojia huenda unaendelea katika Korea Kaskazini.
No comments:
Post a Comment