Search This Blog

Tuesday, October 19, 2021

EU: uamuzi wa mahakama ya Poland ni kitisho kwa utawala wa sheria


Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, amesema uamuzi uliotolewa hivi karibuni na Mahakama ya Katiba nchini Poland unatishia misingi ya Umoja huo na lazima utachukuliwa hatua. 
 
Katika hotuba yake leo bungeni mjini Strasbourg, von der Leyen amesema hukumu hiyo ni kinyume na utawala wa sheria barani Ulaya: Leyen amesema hii ni mara ya kwanza kabisa kwamba mahakama ya nchi mwanachama inasema kuwa mikataba ya Umoja wa Ulaya haiendani na katiba ya kitaifa. 
 
Na hii ina athari kubwa kwa watu wa Poland, kwa sababu uamuzi huo una athari ya moja kwa moja kwenye ulinzi wa mahakama. 
 
Wasiwasi umezuka kwamba kwa uamuzi huu wa Mahakama ya Katiba ya Poland, taifa hilo nalo linaelekea kuchukuwa hatua ya kile kiitwacho Polexit, ama kujitowa kwenye umoja wa mataifa 27 wanachama wa Muungano wa Ulaya, kama ilivyofanya Uingereza, Brexit.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...