Search This Blog

Saturday, October 9, 2021

Austria: Kansela Kurz akataa shinikizo la kujiuzulu


Kansela wa Austria Sebastian Kurz amepuuza tuhuma za ubadhirifu na miito inayomtaka kujiuzulu, na kusema hang'oki katika wadhifa wake. 
 
Katika tangazo lililochapishwa na ofisi yake Ijumaa jioni, Kurz amesema yeye na chama chake sio tu wana uwezo wa kufanya kazi, bali pia wana utashi wa kuhudumu.
 
 Kabla ya tangazo hilo, rais wa shirikisho Alexander Van der Bellen ambaye wadhifa wake ni wa heshima kuliko madaraka, alikuwa amewataka wanasiasa wote nchini humo kuchukuwa hatua sahihi kwa faida ya nchi badala ya maslahi binafsi
 
. Hali kadhalika, chama cha walinzi wa mazingira kinachojumuishwa katika serikali ya muungano, kilibainisha kuwa kuendelea kushiriki kwake kutategemea ikiwa chama cha kihafidhina cha ÖVP kitamchagua kansela mpya muadilifu, kufuatia tuhuma kali za ufisadi dhidi ya Kansela Kurz.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...