Search This Blog

Saturday, September 11, 2021

Yanga kucheza bila mashabiki kesho

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kupitia TFF limetangaza kuwa mchezo wa Yanga dhidi ya River United ya Nigeria wa round ya awali ya club Bingwa Afrika kesho utachezwa bila mashabiki katika uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na tahadhari ya corona.

Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa mechi yao ya kesho Jumapili dhidi ya Rivers United itapigwa bila ya uwepo wa mashabiki.

Ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo utachezwa Uwanja wa Mkapa. Jana Yanga walitoa taarifa kuhusu viingilio vya mchezo huo ila leo wametoa taarifa kwamba hakuna ruhusa ya uwepo wa mashabiki.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa CAF imezuia mashabiki kwa sababu Tanzania bado haijafikia viwango vya shirikisho hilo juu ya protokali za usimamizi wa ugonjwa wa Uviko-19.

Kwa mechi zote ambazo zitachezwa kwa wakati huu hazitakuwa na mashabiki ikiwa ni pamoja na ule wa leo wa Kombe la Shirikisho kati ya Azam FC dhidi ya Horseed FC ya Somalia.

Pia taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imeeleza kuwa imewasiliana na timu zote zinazoshiriki mashindano ya kimataifa ambazo ni Simba, Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Biashara United na Azam FC ambazo zinawakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...