Search This Blog

Saturday, September 18, 2021

Waziri Ummy akagua ujenzi daraja linalounganisha Mwanambaya - Mipeko, Mkuranga


Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kutimiza kauli mbiu yake isemayo TARURA tunakufungulia barabara kufika kusiko fikika imejenga daraja lenye gharama ya shilingi milioni 200 linalounganisha  barabara ya Mwanambaya - Mipeko  katika Halmashauri ya Wilaya ya  Mkuranga, Mkoani Pwani.

Akikagua ujenzi wa Daraja hilo leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu amesema ameridhishwa na kazi ya ujenzi wa daraja la  Mwanambaya – Mipeko  na kuwapongeza TARURA  Halmashauri ya  Wilaya ya Mkuranga  kwa usimamizi wenye weledi katika ujenzi huo

Amesema  kuwa kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani ni kuhakikisha anaimarisha miundombinu vijijini na mijini ili kuwaondolea wananchi  changamoto za  miundombinu  ya barabara  katika maeneo yao.

“Daraja la Mwanambaya –Mipeko ni moja ya madaraja yanayojengwa nchi nzima, kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassani anataka  kufanya mapinduzi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara za vijijini”amesisitiza Waziri Ummy

Waziri Ummy amesema kuwa katika kuhakikisha miundombinu ya vijijini  serikali imeweza kuongeza bajeti ya TARURA kutoka shilingi milioni 275  hadi kufikia shilingi 275 hadi  bilioni 940 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hivyo  amewataka wananchi kutegemea  mabadiliko makubwa katika kutatua kero za miundombinu ya barabara nchini .

Naye Meneja wa Tarura Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Silas Dilliwa amesema kuwa  ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 65 ambapo ukamilishwaji wa daraja hilo kutasaidia  kupunguza adha ya wananchi   hasa katika kipindi cha mvua ambapo wengi wao hushindwa kuvuka katika eneo hilo

Aidha Daraja la Mwanambaya – Mipeko  linajengwa na Mkandarasi M/S JONENAC CONSTRUCTION LIMITED na linatarajiwa kukamilka mnamo tarehe 4/03/2022




 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...