Search This Blog

Sunday, September 12, 2021

Wavuvi waomba kupelekewa chanjo ya Uviko 19


Wavuvi wa ziwa Victoria kutoka visiwa 14 vilivyo wilayani Sengerema wameiomba Serikali kuwapelekea chanjo ya Uviko 19   visiwani humo kutokana na kituo cha kutolea chanjo hicho kuwa mbali na maeneo yao.


Mwenyekiti wa Wavuvi kisiwa cha Gembale, Hassan Mhenga amesema watu wanashindwa kuvuka ziwa kwenda zahanati ya Lushamba kupata chanjo ya Uviko 19, hivyo kuwalazimu kutumia gharama kubwa ya usafiri.


Amesema kama huduma hiyo itafikishwa kwenye Visiwa hivyo watu wengi watajitokeza kupata chanjo hiyo ya Uviko 19 na kujikinga na maradhi hayo.


“Serikali inatakiwa kupeleka chanjo huko Ili kuwasaidia wavuvi," amesema Mhenga.


Mmoja wa Wavuvi Kisiwa cha Nyamango Saimoni Kube amesema wako tayari kupata chanjo hiyo kama Serikali itaona umuhimu wa kuwafikisha huduma hiyo kwenye maeneo yao ya kufanyia kazi.


Soma hapa:Waliopata chanjo ya Uviko - 19 wafikia asilimia 34 ya lengo


Serikali imetenga Vituo vya kutolea chanjo ya Uviko 19 sehemu mbalimba lakini imesahau kupeleka huduma hiyo kwenye maeneo ya visiwani.


Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bulyaheke Jonathani Kuditha ambayo kata yake inamiliki Visiwa 14 amesema wao wamekwishaliona hilo atapeleka  maombi hayo kwenye Mamulaka husika Ili kuona namuna ya kuwasaidia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...