Search This Blog

Saturday, September 11, 2021

Wapenzi wakutwa wamefariki dunia


WATU wawili wanaodhaniwa kuwa ni wapenzi wamekutwa wamefariki huku chanzo kikidaiwa kuwa walikunywa sumu katika Kitongoji cha Mlandizi kata ya Mlandizi Tarafa ya Mlandizi Wilaya ya Kipolisi Mlandizi, mkoani Pwani.

Akizungumzia tukio hilo la kustaajabisha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesme; “Mnamo Tarehe 5 Septemba, 2021 asubuhi huko Mlandizi, watu wawili wanaodaiwa kuwa ni wapenzi walikutwa wamefariki katika makazi yao baada ya kunywa ya kitu kinachodhaniwa ni sumu.

“Watu hao ni Godfrey Pius Mandai (48) ambaye alikuwa ni Dereva wa Kampuni na Veronica Gerald (42), mfanyabiashara na mkazi wa Mtwara ambaye alisafiri kutoka Mtwara na kumfuata mpenzi wake huyo Mlandizi.

“Imedaiwa kuwa mwanaume yule alitengengeza juisi ambayo ndani yake ilikuwa na sumu akampa Veronica akanywa na kufariki, mwanaume huyo alipoona mpenzi wake amefariki na yeye akanywa ile juisi yenye sumu na akafariki.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...