Umoja wa Falme za kiarabu UAE umesema wakaazi wake waliopata chanjo ya corona iliyoidhinishwa na shirika la afya ulimwenguni WHO, wanaweza kurejea nchini kuanzia Septemba 12 kutoka orodha ya mataifa ambayo watu wake walipigwa marufuku kuingia nchini humo.
Dubai inatarajia kufungua maonyesho yake makubwa Oktoba mosi yaliyoahirishwa kwa mwaka mmoja kufuatia janga la corona, na UAE inategemea maonyesho hayo ili kuupiga jeki uchumi wake.
Nchi ambazo watu wake wameidhinishwa kuingia UAE kuanzia septemba 12 ni India, Pakistan, Namibia, Zambia, Congo, Uganda, Afrika Kusini, Liberia, Nigeria, Afghanistan miongoni mwa mataifa mengine.
Hata hivyo ni lazima kwanza kila mmoja kupata idhini kutoka kwa serikali na kufanya vipimo vya corona kabla ya kuingia nchini humo hii ikiwa ni kulingana na taasisi ya kushughulikia masuala ya dharura ya UAE.

No comments:
Post a Comment