Search This Blog

Monday, September 13, 2021

Umoja wa Mataifa kufanya kongamano la kuichangia Afghanistan fedha


Umoja wa Mataifa utafanya kongamano la kuchangisha fedha leo mjini Geneva kwa ajili ya juhudi zake za kuchangisha zaidi ya dola milioni 600 kwa ajili ya Afghanistan. 
 
Umoja huo unaonya kwamba huenda kukawa na mgogoro wa kibinadamu katika nchi hiyo kufuatia Taliban kuchukua madaraka. Kongamano hilo litahudhuriwa na maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Katibu Mkuu Antonio Guterres na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas. 
 
Hata kabla Taliban kuuteka mji wa Kabul mwezi uliopita, nusu ya idadi ya watu nchini Afghanistan au watu milioni 18 walikuwa wanategemea misaada. 
 
Umoja wa Mataifa unatahadharisha kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka kutokana na ukame na uhaba wa fedha na chakula.
 
 Mataifa mengi ya kigeni yamesitisha utpaji wa misaada ya kifedha kwa Afghanistan kufuatia Taliban kuchukua madaraka jambo lililouwekea shinikizo kubwa Umoja wa Mataifa.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...