Search This Blog

Sunday, September 19, 2021

Ufaransa yaiokosoa Australia kwa kufutilia mbali ununuzi wa nyambizi

 


Balozi wa Ufaransa nchini Australia Jean-Pierre Thebault amesema jana kuwa Australia imefanya kosa kubwa la kidiplomasia kwa kufuta makubaliano ya kununua nyambizi za Ufaransa za mabilioni ya dola na kuingia katika mkataba mbadala na Marekani na Uingereza. 

Kabla ya kurejea nchini Ufaransa, Thebault aliwaambia wanahabari nchini Australia kwamba hatua hiyo ilikuwa kosa kubwa na ushughulikiaji mbaya wa ushirikiano kwasababu ununuzi huo wa nyambizi haukuwa mkataba bali ushirikiano ambao ulitakiwa kutegemea uaminifu, makubaliano ya pamoja na ukweli. 

Siku ya Alhamisi, Australia ilitangaza kwamba itafutilia mbali makubaliano ya mwaka 2016 na kampuni ya manowari ya Ufaransa, kutengeneza nyambizi za kawaida na badala yake kutengeneza nyambizi zisizopungua nane zenye uwezo wa kinyuklia kwa kushirikiana na Marekani na Uingereza baada ya mataifa hayo matatu kuingia katika makubaliano ya ulinzi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...