Manchester United bado wameonesha utayari wa kupata saini ya mchezaji wa Borussia Dortumund na raia wa Norway kiungo Erling Braut Haaland, mwenye miaka 2, licha ya kurudi mchezaji machachari raia wa Ureno Cristiano Ronaldo,36.
United pia inaangalia kwa ukaribu kumsainisha Jude Bellingham baada ya kumvutia kiungo huyo wa Uingereza katika ziara waliyoifanya kablahajaamua kuhamia Borussia Dortmund.
Lionel Messi, 34, atapata £25.6m katika misimu miwili ijayo akiwa na Paris St-Germain, Mchezaji huyo raia wa Argentina mshahara wake unatarajiwa kuongezeka zaidi mpaka kufikia £8.5m katika kipindi cha miaka mitatu.
Wakala wa mchezaji Matthijs de Ligt Mino Raiola anasema kuwa beki huyo wa kati wa Uholanzi anaweza kuondoka Juventus mwishoni mwa msimu, huku Chelsea imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 22.
Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Edinson Cavan ameonesha nia yake ya kutoondoka Old Trafford licha ya kwamba mchezaji huyo raia wa Uruguay kugombania namba na Ronaldo.
Chelsea imeonesha nia ya kutoa ofa nzuri kwa kiungo wa Monaco Aurelien Tchouameni,21, kujiunga na Stanford Bridge,Trhuku Juventus nao wameonekana kuvutiwa na mchezaji huyo raia wa ufaransa.
Bosi wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amekubali kwamba bado hajaamua mlinda mlango yupi atakuwa chaguo lake la kwanza msimu huu, kati ya David de Gea 30 wa Uhispania na Dean Henderson, 24 wa Uingereza.
Mlinzi wa Aston Villa Matty Cash anatakiwa na Poland kabla ya raundi inayofuata ya kufuzu Kombe la Dunia kwa sababu mchezaji huyo wa miaka 24 ameonesha utayari wake wa kuchezea nchi ya upande wa mama yake.
Kocha wa Wolverhampton Wanderers, Bruno Lage amevionya vilabu vya Manchester United na Arsenal kuwa hatamruhusu kiungo wa Ureno Ruben Neves, 24, aondoke bila ya kumalza michezo yake.
Kipa wa Liverpool Alisson anasema angependa kujiunga tena na timu ya Brazil ya Internacional ikiwa atapewa nafasi, lakini mchezaji huyo wa miaka 28 ni "mwenye furaha" baada ya hivi karibuni kusaini kandarasi ya miaka sita huko Anfield.
Kocha mkuu wa Barcelona Ronald Koeman anafikiria kumuacha beki wa pembeni wa Uhispania Sergi Roberto, 29, hasa kwenye mchezo wa Jumatatu dhidi ya Granada ili kumlinda baada ya kuzomewa uwanjani siku ya Jumanne walipopoteza dhidi ya Bayern Munich.











No comments:
Post a Comment