Mshambuliaji wa Norway na Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 21, hana nia ya kuharakisha uamuzi kuhusu hatma yake ya baadaye wakati kifungu cha kumwezesha kuondoka kitaanza kutekelezwa mwaka 2022. (90 Min)
Manchester City wamemuongeza Jude Bellingham wa Borussia Dortmund kwenye orodha ya wachezaji wanaowasaka na watamenyana na Liverpool kumpata kiungo huyo wa kati wa England aliye na miaka 18. (Star on Sunday)
Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti anasema "hakuna majuto" katika klabu hiyo baada ya juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kutoka Paris St-Germain katika msimu wa joto. (Goal)
Arsenal wanamlenga kocha wa Leicester City Brendan Rodgers na mkufunzi wa Nice Christophe Galtier kama chaguo lao endapo wataamua kumfurusha Mikel Arteta. (Transfer Window Podcast, via Teamtalk)
West Ham wanamfuatilia kiungo wa kati wa Preston North End Lewis Leigh, huku Everton pia wakielekeza darubini yao kwa mchezaji huyo wa Uingereza aliye na miaka 17. (Football Insider)
Mkufunzi wa Chelsea Thomas Tuchel anasema "tulifanya uamuzwa busara" kutomuachilia winga wa England Callum Hudson-Odoi, 20, kuondoka siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji. (Football London)
Mkataba wa kiungo mshambuliaji wa Millwall Jed Wallace unamalizika msimu ujao na mchezaji huyo wa miaka 27 wa Uingereza ananyatiwa na Brentford, Burnley, Crystal Palace, Newcastle United, West Ham Pamoja na Celtic, Rangers naWest Brom. (Football League World)
Chelsea wamefanya mazungumzo ya kumsajili kinda matata wa Ujerumani Karim Adeyemi, 19, miaka mitatu iliyopita hawajafanikiwa kumpata mshambuliaji huyo wa Red Bull Salzburg. (Sunday Express)
Barcelona imekataa kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 24, na beki wa Ivory Coast Serge Aurier, 28, kama sehemu ya mkataba wa kumuuza mchezaji wao Emerson Royal kwa Tottenham. (Fabrizio Romano, via Sunday Express)
Mkurugenzi wa michezo wa Ajax Marc Overmars anasema yuko radhi kutekeleza jukumu lake la sasa katika klabu ya Barcelona badala ya Arsenal. (Ajax Life, via Marca)










No comments:
Post a Comment