Search This Blog

Sunday, September 5, 2021

Tetesi za Soka Kimtif


Liverpool wanaendelea kuzungumza na wawakilishi wa Mohamed Salah kuhusu mkataba mpya wa mshambuliaji nyota huyo wa Misri aliye na miaka 29. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa Everton na Colombia James Rodriguez amehusishwa na uhamisho wa kwenda Istanbul Basaksehir, klabu hiyo ya Uturuki inapania kumsajili mchezaji huyo wa miaka 30- kabla ya dirisha lao la uhamisho kufungwa Jumatano wiki hii. (Footmercato - in French)

Mkufunzi wa Sevilla Julen Lopetegui anasema klabu hiyo ya La Liga huenda ikamzuia beki Mfaransa Jules Kounde, 22, kuhamia Chelsea msimu huu wa joto. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Arsenal kutoka Misri Mohamed Elneny anaendelea kuhusishwa na tetesi za uhamisho wa kwenda Besiktas, lakini mashariti ya marupurupu ya mchezaji huyo wa miaka 29- yanasemekana kuchangia kusambaratika kwa mpango huo. (Mirror)

Mkurugenzi wa soka wa Ajax Marc Overmars amesema kipa wa Cameroon Andre Onana, ambaye anasakwa na Arsenal, huenda akaondoka msimu ujao kwa mkataba wa bila malipo. (Team Talk)

Mabingwa wa Italia Inter Milan huenda pia wakamnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25-wanapomtafuta atakayemrithi kipa wa Slovenia Samir Handanovic, 37. (Calciomercato - in Italian)

Paris St-Germain wana matmaini kwamba mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe atajitolea kikamilifu kutekeleza mkataba wake mpya licha ya azma ya kiungo huyo wa miaka ya 22-kutaka kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Athletic - subscription required)

Arsenal inakabiliwa na hatari ya kupata hasara kubwa baada ya kushindwa kumuuza mshambuliaji wa miaka 22 Eddie Nketiah , huku mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa England wa chini ya miaka 21 akikataa ofa ya kandarasi kutoka kwa Gunners. (Sun)

Kiungo wa kati wa Huddersfield Town Muingereza Lewis O'Brien ,22, ambaye pia alitakiwa na Leeds United msimu uliopita, anajadiliana na Terriers kuhusu mkataba mpya. (Huddersfield Examiner)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...