Search This Blog

Tuesday, September 7, 2021

Tetesi za soka kimataifa


Hatua ya Liverpool kushindwa kumuuza winga wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 29, au mshambuliaji wa Ubelgiji wa miaka 26- Divock Origi imewafanya wakose nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Patson Daka, 22, wa Zambia kutoka Red Bull Salzburg, kabla ajiunge na Leicester City. (Here We Go Podcast, via Express)

Kiungo wa kati wa England Jude Bellingham, 18, amedokeza kuwa huenda akajiunga na Liverpool huku mkufunzi Jurgen Klopp akijiandaa kuvamia klabu yake ya zamani ya Borussia Dortmund. (Star)

Liverpool pia wamepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa wa miaka 27 wa Genk na Nigeria Paul Onuachu na mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Mbelgiji huyo. (Mirror)

Reds pia ni miongoni mwa klabu tatu ikiwemo Bayern Munich na Barcelona zinazopania kumsajili nyota kinda wa Red Bull Salzburg na Ujerumani Karim Adeyemi, 19, ambaye amefunga mabao sita katika mechi sita za Ligi Kuu msimu huu. (Bild, via Mirror)

Chelsea wataendelea kumfuatilia mchezaji wa Sevilla wa safu ya kati na nyuma wa Jules Kounde, 22, kwa lengo la kumnunua mwezi Januari baada ya kumkosa mlinzi huyo msimu huu wa joto. (Evening Standard)

Manchester City imemkosa Wesley Ribeiro Silva msimu huu baada ya dao lao la £6.5m la kumnunua winga wa Brazil wa miaka 22 kukataliwa na Palmeiras. (Marca, via HITC)

Arsenal wamekataa dau iliyowsilishwa na klabu ya Uturuki ya Galatasaray kumnunua kiungo wa kati wa Misri Mohamed Elneny,29. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Marco Asensio, 25, amekataa nafasi ya kujiunga na Tottenham au AC Milan msimu huu wa kiangazi, baada Mhispania huyo kudokeza kuwa hajatulia Real Madrid. (Marca)

Manchester United wamepewa nafasi ya kumsaini kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 22, msimu ujao baada ya Chelsea kuelekeza darubini yao kwa mchezaji mwingine. (Mirror)

Mlinzi wa Arsenal aliyesahaulika Mgiriki Konstantinos Mavropanos, 23, huenda akapewa mkataba wa kudumu katika klabu ya Stuttgart ambyo sasa anaichezea kwa mkopo. (Bild, via Star)

Kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 30, amekataa ofa kadhaa za kuondoka Juventus wakati wa msimu wa kiangazi kwani anatarajia kuwa katika kikosi cha kwanza chini ya ukufunzi wa Massimiliano Allegri. (Calciomercato - in Italian)

Manchester City na PSG wanamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto na nyuma wa AC Milan ana Ufaransa Theo Hernandez, 23. (Calciomercato - in Italian)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...