Manchester United bado wanamtaka mchezaji wa West Ham wa safu ya kati Muingereza Declan Rice,22, ijapokuwa hawakumnunua msimu huu wa joto. (ESPN)
Liverpool wanatafakari uwezekano wakumnunua kiungo wa kati wa Valencia na Uhispania Carlos Soler, ambaye ana kifungu cha kutolewa cha pauni milioni 125 katika mkataba wake. Kocha wa Reds Jurgen Klopp anataka Soler kuchukua nafasi ya kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ambaye alijiunga na Paris St-Germain kwa mkataba wa bila malipo msimu huu wa kiangazi. (Fichajes - in Spanish)
Liverpool pia wanamtaka mshambuliaji wa Uhispania Marco Asensio,25, ambaye anajiandaa kuondoka Real Madrid katika juhudi za kuzindua upya taaluma yake. (Todofichajes - in Spanish)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Manchester United Donny van de Beek anasema amefanya mazungumzo na Everton kuhusu uwezekano wa uhamisho waw a mchezaji huyo wa Uholanzi wa miaka 24. (Express)
Hata hivyo, Van de Beek anasema Ole Gunnar Solskjaer anataka sana asalie Old Trafford baada ya kufanya mazungumzo na kocha huyo wa United kuhusu hatma yake ya baadaye. (Vibe with Five)
PSG wameelekeza darubini yao kwa kiungo matata wa safu ya kati ya AC Milan na Ivory Coast Franck Kessie, 24, kwa wanaamini mchezaji nyota wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, angelipendelea kuhamia Real Madrid msimu ujao. (Defensa Central - in Spanish)
Tottenham pia wanamtaka Kessie na huenda wakamuuza kiungo wa kati wa Ufaransa wa miaka 24 Tanguy Ndombele ili kufanikisha ndoto hiyo. (Express)
Pendekezo la kiungo wa Arsenal wa safu ya kati Mohamed Elneny kuhamia Besiktas limegonga mwamba kutokana na matakwa ya hali ya juu ya marupu rupu ya hali juuya mchezaji huyo wa Misri wa miaka 29. Elneny,ambaye alikuwa Besiktas kwa mkopo msimu wa 2019-20, pia alishidwa kuhamia also saw a Galatasaray kutokana na sababu hiyo hiyo. (talkSPORT)
Kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 30, amekataa ofa kadhaa za kuondoka Juventus wakati wa msimu wa kiangazi kwani anatarajia kuwa katika kikosi cha kwanza chini ya ukufunzi wa Massimiliano Allegri. (Calciomercato - in Italian)
Phil Foden, 21, anajiandaa kupewa ofay a mkataba mpya Manchester City licha ya kiungo wa kati huyo wa England kusalia na miaka mitatu katika mkataba wake wa sasa. (Manchester Evening News)
Atletico Madrid huenda wakachukua hatua ya kumsajili kipa wa Argentina wa miaka 29- Emiliano Martinez kutoka Aston Villa ikiwa mchezaji wa kimataifa wa Slovenia Jan Oblak, 28, ataagana na mabingwa hao wa La Ligamsimu ujao wa joto. (La Razon - in Spanish)
Manchester City na PSG wanamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto na nyuma wa AC Milan ana Ufaransa Theo Hernandez, 23. (Calciomercato - in Italian)
Inter Milan wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa Corentin Tolisso, 27, kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake na Bayern Munich utakapomalizika msimu ujao. (Tuttosport via Sempre Inter)

No comments:
Post a Comment