Arsenal itamtoa mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, kwa Sevilla kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Morocco wa miaka 25 Youssef En-Nesyri. (La Razon - in Spanish)
Leeds United wameanza mazungumzo ya mkataba na kiungo wa kati wa England Kalvin Phillips kwa nia ya kutompoteza mchezaji huyo wa miaka 25 kwa wapinzani wao Manchester United. (Star)
Tottenham wanamtaka kipa wa West Brom na England Sam Johnstone, 28. (Football Insider)
Spurs pia wamesema wako tayari kumwachilia kiungo wa kati wa England Harry Winks, 25, kuondoka mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. (Caughtoffside)
Kiungo wa kati wa England Declan Rice amesema anaridhika kuwa West Ham na anaweza kufikia malengo yake katika klabu hiyo. Rice mwenye umri wa miaka 22-amehusishwa na tetesi za kujiunga na Chelsea na Manchester United. (Sky Sports)
Manchester City wanamnyatia kiungo wa kati wa Bayern Leverkusen wa miaka 18- Mjerumani Florian Wirtz. (Bild via Sport Witness)
Chelsea wanafikiria kumleta mlinzi wa Villarreal Pau Torres, 24, katika klabu hiyo. Manchester United pia wanamtaka Mhispania huyo. (90min)
Inter Milan hawataki kumsaini kipa wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 29. Klabu hiyo ya Serie A badala yake inamsaka mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Andre Onana,25 wa Ajax. (Fabrizio Romano via Twitter)
Leno anaamini sababu ya kuachwa nje ya kikosi cha kwanza cha Gunners hivi karibuni sio utendakazi wake na anataka kuondoka mwezi Januari. (Bild via Mirror)
Kiungo wa Ufaransa wa safu ya kati na nyuma Jules Kounde anasema atazingatia Sevilla baada ya dau la Chelsea kushindwa kumsaini mchezaji huyo wa miaka 22-wakati wa kiangazi. (Star)
Rais wa Fiorentina Rocco Commisso anasema klabu hiyo inajizatiti kumshawishi Dusan Vlahovic ambaye pia ananyatiwa na Arsenal na Chelsea kusaini mkataba mpya. Mshambuliaji huyo wa Serbia wa miaka, 21, alifunga mabao 21 ya Serie A msimu uliopita. (Express)
Everton wanamfuatilia kiungo wa kati wa Roma Gonzalo Villar 23-baada ya kubaini kuwa mchezaji huyo hayupo katika mipango ya kocha Jose Mourinho ya klabu hiyo. (Fichajes - in Spanish)
No comments:
Post a Comment