Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu. (Le10 Sport - in French)
Chelsea wanataka kumsajili beki wa kati wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 22. (Mirror)
FC Basel inafikiria kumchukua mlinda lango wa Liverpool na Ujerumani Loris Karius, 28. (Bild - in German
Barcelona italazimika kulipa euro milioni 1.8 (£ 1.5m) ili kumtoa Roberto Martinez kutoka kwa mkataba wake na timu ya taifa ya Ubelgiji. (Sport - in Spanish)
Lakini Martinez amepuuza ripoti zinazomuhusisha na kazi hiyo kama mbadala anayeweza kuchukua nafasi ya Mholanzi aliye chini ya shinikizo Ronald Koeman, 58. . (Eurosport)
Bayern Munich wana nia ya kumsajili beki wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, lakini mchezaji huyo wa miaka 28 anataka kusaini mkataba mpya huko Stamford Bridge. . (Bild - in German)
Liverpool wanamtazama winga wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 25 (Fichajes - in Spanish)
Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amedokeza kwamba kiungo wa England Ruben Loftus-Cheek, 25, anapaswa kumvutia ili kuokoa maisha yake ya Blues (Express)
Manchester City wamekataa dau la pauni milioni 15 kutoka Borussia Dortmund kwa mshambuliaji wa Uingereza Liam Delap, 18 (Football Insider)
Arsenal na AC Milan wana nia ya kumsajili winga wa Uholanzi wa Club Brugge Noa Lang, 22. (Express)
Skauti wa Barcelona wamemtazama mlinda mlango wa Brighton Carl Rushworth, 20, ambaye kwa sasa yuko mkopo huko Walsall. (Mirror)

No comments:
Post a Comment