Search This Blog

Sunday, September 26, 2021

Tetesi za soka kimataifa


Chelsea wanajiandaa kuwasilisha dau la euro milioni 120 sawa na (£102m) kumnunua mlinzi wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 22. (AS - in Spanish)

Lakini Chelsea inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Juventus kumpata kiungo wa kati wa AS Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni,21. (Calciomercato - in Italian)

Mshambuliaji wa Aston Villa na England Ollie Watkins, 25, yuko katika orodha ya chaguzi za Tottenham. (Fichajes - in Spanish

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic amejitenga klabu hiyo na tetesi zinazowahusisha na usajili wa mchezaji wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger,28. (DAZN, via Goal)

Tottenham ilikuwa na makubaliano ya kanuni kumsajili mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Uhispania Pau Torres kutoka Villarreal msimu huu wa joto, lakini kiungo huyo wa miaka 24 "amependelea kusubiri ofa nzuri zaidi ". (AS - in Spanish)

Manchester City wanapania kumsajili kiungo wa kati wa RB Leipzig Mfaransa Christopher Nkunku, 23. (Fichajes, via TEAMtalk)

Mshambulialiji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21 anayenyatiwa na Manchester City, anajiandaa kufanya mazungumzo mapya Fiorentina. (DAZN, via Manchester Evening News)

Leicester City wameonesha nia ya kutsks kumsajili kiungo wa kati wa Lazio Mhispania Luis Alberto, 28. (Fichajes - in Spanish)

Mmiliki mwenza wa Manchester United Joel Glazer amedokeza kuwa klabu hiyo itaendelea kutumia fedha nyingi, akisema "kuns mengi zaidi ya kufanywa here". (Sun)

Juventus wanatafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Dortmund na ubelgiji Axel Witsel, 32 mwezi Januari mwakani. (Calciomercato - in Italian)

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke anasema ukosefu wa muda wa kucheza unamkabili winga wa England Jadon Sancho, 21, Manchester United "unaniumiza moyo". (Sport1, via Express)

Cristiano Ronaldo anataka kustaafu akiwa katika klabu ya Manchester United. Mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka The 36- kisha anataka jukumu la ukufunzi kstiks klsbu hiyo. (Sun)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...