Search This Blog

Saturday, September 25, 2021

Tetesi za soka kimataifa


Manchester United inasaka mbadala wa kiungo wa England mwenye umri wa miaka 22 Declan Rice kufuatia dau kubwa la £80-90m wanalolitaka West Ham (ESPN)

Antonio Rudiger anaweza kujizolea mshahara wa £400,000 kwa wiki kama ataikacha Chelsea, huku vilabu vya Bayern Munich na Juventus vikiwa tayari kumpa mshahara huo mnono mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 28 kutoka ule wa £130,000 kwa wiki anaolipwa sasa na Chelsea. (Mirror)

Borussia Dortmund wanamfuatilia mshambuliaji wa Manchester United mfaransa Anthony Martial, 25, kama mbadala wa mshambuliaji wake raia wa Norway Erling Braut Haaland, 21. (90min)

Manchester City wanataka kuipiku Real Madrid  katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain mfaransa Kylian Mbappe, 22 msimu ujao. (Transfer Window, via Mail)

Real Madrid ilikataa ofa ya Arsenal ya £34m ya kumsajili kiungo wake raia wa Hispania Marco Asensio,25, msimu huu. (Cadena Ser, via Mirror

Atletico Madrid wanamtaka mshambuliaji wa Arsenal na England mwenye umri wa miaka 22 Bukayo Saka. (La Razon, via Star)

Chelsea itataka wachezaji wanne kutoka Real Madrid kama mpango wa kumruhusu mlinzi wa kulia Muingereza Reece James 21. (Express)

Chelsea itaachana pia na mpango wake wa kumuwania mlinzi wa kifaransa kutoka Sevilla Jules Kounde, 22, na mlinzi wa kati wa PSG mbrazil Marquinhos, 27, ili kuelekeza nguvu zake za kumsajili mlinzi wa Juventus na Uholanzi mwenye umri wa miaka 22 Matthijs de Ligt. (Star)

Juventus wanaendelea na mazugumzo na mshambuliaji raia wa Argentina Paolo Dybala, 27, kuhusu mkataba mpya ulioboreshwa zaidi. (Calciomercato - in Italian)

Barcelona watamuuza kiungo wake mchezeshaji raia wa Brazil Philippe Coutinho, 29, katika dirisha la usajili la Januari. (Marca - in Spanish

Nyota wa zamani wa Barcelona Xavi Hernandez huenda akachukua nafasi ya kocha Ronald Koeman aliye kwenye shinikizo la kuondolewa klabuni hapo. (Marca - in Spanish)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...