Search This Blog

Sunday, September 19, 2021

Tetesi za Soka KIMATAIFA


Barcelona wanajiandaa kuwasilisha ofa za kuwanunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, nyota wa Ufaransa na man united Paul Pogba, 28, na mchezaji wa Uhispania Dani Olmo, 23. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Huku mkataba wa Pogba wa Manchester United ukikamilika majira yajayo ya joto , kilabu hiyo imejiandaa kutoa ofa ya Pauni 400,000 kwa wiki kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara wa juu zaidi katika Ligi Kuu ya England wakati wote. (Express)

Kiungo Jesse Lingard, 28, na beki Eric Bailly, 27, ni miongoni mwa wachezaji saba ambao wanaweza kuuzwa na Manchester United mwezi Januari. (Sun)

Chelsea itakabiliana ana kwa ana na Juventus kupata saini ya kiungo wa chini ya umri wa miaka 21 wa Ufaransa na Monaco Aurelien Tchouameni, 21, mnamo Januari. (Tuttomercatoweb - in Italian)

Liverpool, Tottenham na Juventus wamepania kupigania winga wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman, 25. (Fichajes - in Spanish)

Chelsea pia inavutiwa na Coman baada ya mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Bayern Munich kumtaka aondoke klabuni. (Mirror)

Bosi wa Barcelona Ronald Koeman hajui hatma yake iko vipi wakati kukiwa na ripoti kwamba rais Joan Laporta anaunda orodha ya watu wanaochukua usukani wa kilabu hiyo (Express)

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 28, anaweza kuwa bado anahisi athari za uhamisho wake ulioshindwa kufanyika wa Manchester City msimu huu wa joto. (TalkSport)

Juventus walikuwa wamepanga kumsaini Gianluigi Donnarumma, 22, bila malipo kutoka AC Milan msimu huu wa joto, lakini walilazimika kujiondoa kwa sababu za kifedha, na kuiruhusu Paris St-Germain kumchukua (Goal)

Mkurugenzi wa michezo wa PSG Leonardo amepuuza maoni kwamba nyota wa Argentina Lionel Messi, 34, atapata zaidi ya pauni milioni 30 kwa msimu wakati wa mkataba wake wa miaka mitatu. (Mail)

Manchester United inawasiliana na kiungo wa England Jesse Lingard, 28, juu ya mkataba mpya. Bruno Fernandes na Luke Shaw pia wako kwenye 'orodha ya wanaozingatiwa kwa mkataba' na kilabu hiyo . (Fabrizio Romano)

Arsenal inaandaa dau la pauni milioni 20 kwa Winga wa Uholanzi mwenye chini ya umri wa miaka 21 na winga wa Club Bruges Noa Lang, 22. (Fichajes via Mirror)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...