Search This Blog

Saturday, September 18, 2021

Tetesi za Soka kimataifa


Barcelona ina mpango wa kujaribu kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa England na Manchester City Raheem Sterling, 26, mwezi Januari baada ya kushindwa kumleta Nou Camp majira ya joto. (Sport - in Spanish)

Ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola anasema kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28-huenda akajiunga tena na Juventus wakati mkataba wake na Manchester United utakapomalizika mwisho wa msimu huu. (Rai Sport via Corriere dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji wa Inter Miami Gonzalo Higuain anasema klabu hiyo ya MLS ina ndoto ya kumsajili Lionel Messi wakati mkataba wa nyota huyo na Paris St-Germain itakapomalizika mwaka 2023. (ESPN Argentina - in Spanish)

Liverpool wameanzisha mazungumzo ya kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita,26. Kandarasi yake ya sasa inamalizika mwaka 2023. (Calciomercato - in Italian)

Mhambuliaji Kayky, 18, raia wa Brazil ameanza kufanya mazoezi na Manchester City baada ya klabu hiyo kusongeza mbele uhamisho wake kutoka Fluminense, ambao awali ulikuwa ukamilishwe Januari. (Manchester Evening News)

Tottenham huenda wakafufua upya mpango wao wa kumsaka beki wa Ujerumani Antonio Rudiger mkataba wake na Chelsea usiporefushwa msimu ujao. (Express)

Mkufunzi wa Chelsea Thomas Tuchel anasema kuna "sababu nyingi " ya Rudiger kuondoka lakini beki huyo wa kati hajatilia maanani uvumi unaoendelea. (Mail)

Tuchel amepuuzilia mbali tetesi kuwa Chelsea ilijaribu kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane, 28, kutoka Tottenham, lakini akasema alitarajia atajiunga na Manchester City.(Guardian)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 30- Alexandre Lacazette, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu ujao, atakuwa kiungo ''muhimu''kwa kikosi chake msimu huu . (Metro)

Kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, "amechoka" na uhamisho wake kwenda Paris St-Germain kutoka Liverpool ulikuwa "makosa", kulingana na mwandani wake wa karibu. (L'Equipe - in French)

Mlinzi wa Uhispania Sergi Roberto, 29, atasaini kandarasi mpya na Barcelona wiki chache zijazo baada ya kufikia mkataba na rais wa klabu hiyo Joan Laporta. (Marca)

Winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 20, anafiria kubadili uaminifu wake wa kimataifa kutoka England na kwenda Ghana. (Mail)

Kocha wa Burnley Sean Dyche ana matumaini wachezaji kadhaa watasalia katika klabu hiyo kufuatia hatua yake ya kusaini kandarasi. (Times - subscription required)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...