Search This Blog

Wednesday, September 15, 2021

Tetesi za soka kimataifa


Liverpool imejitokeza kama mojawapo ya klabu ambazo zinamsaka mshambuliaji wa Poland na Bayern Munich Robert Lewandowski ,33, ambaye anatarajiwa kuondoka katika Bayern Munich msimu ujao.. (Fichajes, in Spanish)

Manchester United wamekuwa na mazungumzo mazuri na kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes tangu mwezi Julai. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anataka kusalia Old Trafford na kandarasi yake inachukuliwa na umuhimu mkubwa pamoja na kiungo wa kati Paul Pogba, 28. (Fabrizio Romano via Twitter)

United ilitaka kufanya mazungumzo ya makubaliano na Napoli ili kumsajili nahodha wa Senegal Kalidou Koulibaly, 30, msimu ujao lakini hawakuwa tayari kukubali thamani ya mchezaji huyo kama inavyodaiwa na klabu hiyo ya Serie A ya £34m kumnunua beki huyo wa kati. (Corriere dello Sport via Express)

Liverpool ipo katika nafasi nzuri kuwasilisha ombi la mwezi Januari kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Karim Adeyemi, 19, kutoka klabu ya Austria Red Bull Salzburg. (Mundo Deportivo, in Spanish)

Beki wa Chelsea Antonio Rudiger huenda akauzwa ili kufadhili ununuzi wa beki wa Sevilla Jules Kounde . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Ujerumani ananyatiwa na klabu za PSG na Real Madrid , lakini ameonekana kuwa kiungo muhimu wa safu ya ulinzi wa mkufunzi Thomas Tuchel. (Football 365)

Barcelona ilimnyatia mshambuliaji wa Leeds Rodrigo, 30 katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho msimu huu , lakini klabu hiyo ya ligi ya Premia ikakataa ofa hiyo ya raia huyo wa Uhispania.. (The Athletic, subscription required)

Mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez ameripotiwa kukaribia kutia saini kandareasi mpya na klabu hiyo ya Serie A , ikimaanisha kwamba Arsenal, na Tottenham watalazimika kutumia kitita kikubwa cha fedha iwapo wataamua kuimarisha hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.. (Gazzetta dello Sport, in Italian)

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Jack Wilshere hataki makubaliano ya kulipwa kwa mechi atakazoshiriki katika uwanja wa Emirates baada ya mkufunzi Mikel Arteta kumruhusu kushiriki mazoezi katika uwanja wa timu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameichezea England mara 34 lakini amekosa klabu tangu alipoondoka Bournemouth mapema mwaka huu.. (Metro)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...